Jumapili 21 Desemba 2025 - 15:08
Kikao cha kielimu “Kudhihiri Nuru ya Bibi Fa'timah Zahra (s.a) Katika Zama Zote” Chafanyika Nchini Senegali

Hawzah/ Sambamba na maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Bibi Fa'timah Zahra (a.s), Jumuiya ya Wanawake wa Fatima Zahra (s.a.), inayohusishwa na Baraza la Wanazuoni wa Ahlul-Bayt (a.s.) nchini Senegal, iliandaa kikao cha kielimu chenye anuani isemayo “Kudhihiri Nuru ya Fatima Zahra (s.a.) katika zama zote”, huku kundi la wanawake wanaojihusisha kikamilifu na shughuli za kitamaduni, kielimu na kijamii, jijini Dakar likishiriki.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kikao hiki cha kielimu kilifanyika kwenye makao makuu ya Baraza la Wanazuoni wa Ahlul-Bayt (a.s.) nchini Senegal, kwa ushiriki wa wanawake wasomi na wanaharakati katika nyanja mbalimbali za kijamii na kitamaduni. Programu ilianza kwa usomaji wa aya tukufu za Qur’ani Tukufu uliotekelezwa na Bi Zaynab Jigin.

Baadaye, Bi Maymuna Faye, Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wanawake wa Fatima Zahra (s.a.) na miongoni mwa wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha al-Mustafa (s.w.t.) – tawi la Mashhad Tukufu, aliwakaribisha washiriki na kuwaeleza kuwa; lengo la kuandaliwa kwa kikao hiki ni kubadilishana fikra na kuchunguza njia za kunufaika zaidi na utamaduni wa Kifatimiyya katika maisha ya kisasa.

Kisha, wahutubiaji wakuu waliwasilisha mitazamo yao. Bi Fatima Dimba Bah, mwanaharakati wa vyombo vya habari na mtangazaji wa redio ya Kayar, alikuwa mhutubiaji wa kwanza wa kikao hiki, ambapo alifafanua mada ya “Kuzaliwa na malezi ya Bibi Fatima Zahra (s.a)”.

Katika hatua iliyofuata, Bi Fatima Ghi, mwalimu wa shule ya sekondari, alihutubia kuhusu mada ya “Bibi Fatima Zahra (s.a), kielelezo cha mwanamke Mwislamu”. Aidha, Bi Fatima Waran Bah, mwalimu mwingine wa shule ya sekondari, alichambua vipengele vya kijamii na kibinadamu vya maisha ya Bibi Zahra (s.a), akisisitiza maadili kama vile kupigania haki, kuwatetea waliodhulumiwa na kuitumikia jamii ya wanadamu.

Sehemu ya mwisho ya kikao ilihusishwa na mazungumzo ya pamoja, uwasilishwaji wa mitazamo mbalimbali, pamoja na kipindi cha maswali na majibu kati ya washiriki na wahutubiaji. Hatimaye, baada ya kutolewa zawadi kwa wanawake waliobobea, duka la “Manukato ya Fatima Zahra (s.a.)”, linalosimamiwa na Jumuiya ya Wanawake, lilifunguliwa rasmi.

Ikumbukwe kwamba kikao hiki cha kielimu kilirushwa katika vyombo kadhaa vya televisheni pamoja na mitandao ya habari ya nchini Senegal.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha